FILAMU ya Magic Money , au pesa za
za maajabu iliyotua sokoni mapema wiki hiiimeendelea kuonesha makali ya wasanii Badra ,
Davina na Hemedi.
Ndani ya filamu hiyo Davina anaonekana akitaka
kujua kwa nini mumewe anamkataza kuingia katika
moja ya chumba kilichopo kwenye numba yao.
Chumba hicho ndicho kilichokuwa na pesa za maajabu
lakini Davina hakuwa akielewa kilichokuwemo ndani ya
chumba hicho hali iliyomlazimu kutumia mbinu mbali mbali
ili aweze kuingia na kujua kilichomo .
Siri iliyokuwemo ndani ya chumba hicho ni kwamba ,
mumewealirithishwa pesa hizo ambazo asili yake ni uchawi
hivyo zilipaswa kuhifadhiwa katika chumba cha pekee.
Kierehere cha kutaka kujua kilichomo ndani ya chumba hicho
kinamsukuma Davina kuchonga funguo ya bandia na kuingia ndani ya chumba hicho haamini macho yake , ni tatizo linalo
tengeneza kichwa cha habari cha filamu hiyo.
Mb ali na Davina na Hemedi ,wasanii wengine walioshiriki
katika filamu hiyo pamoja na Badra na Daudi MIchaeli.Source http://www.pilipilimoviehouse.blogspot.com.
Comments