KUHUSU VURUGU, FUJO, VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI, KUNYANYASWA , KUDHALILISHWA NA KUPIGWA WANANCHI WASIO NA HATIA.
Sifa zote njema anastahiki Allah (S.W) Muumba wa mbingu na ardhi na
vyote vilivyomo. Sala na salamu zimfikie kipenzi cha Umma Mtume Muhammad
(S.A.W) jamaa zake, Maswahaba zake na wale wote wanaowafuata kwa wema
hadi siku ya malipo.
Kwa mara nyengine tena nchi yetu imetumbukia katika vitendo vya vurugu,
fujo, uharamia na vitendo vya uvunjifu wa amani kuanzia tarehe 17 hadi
19 Octoba 2012 kufuatia kutoweka kwa Sheikh Farid Hadi katika mazingira
ya kutatanisha.
Vikundi vya Maharamia kwa kutumia kichaka cha kutekwa “Sheikh Farid
Hadi” walitekeleza hujuma kubwa sana ambayo imepelekea maafa kadhaa
ikiwemo kumwaga damu za watu, kuharibiwa mali za watu, kutia khofu kubwa
wananchi, kuashiria kusambaratika kwa Umoja, kuvunja heshima za watu,
na kuharibiwa kwa miundo mbinu.
JUMAZA kama ilivyotangulia kusema kufuatia vurugu na fujo katika
uchaguzi mdogo wa Bububu, kuwa kipo kikundi cha watu wanaotekeleza
mipango yao ya kuihujumu Zanzibar kwa kupinga Serikali ya Umoja wa
Kitaifa ( SUK ) ili kuwarejesha Wazanzibari katika maisha ya hasama na
uadui baina yao pamoja na kupinga harakati za kupigania hadhi ya
Zanzibar ndani na nje, Kimataifa. Kutokana na tatizo hili linaloendelea
kukua na katika kuiangamiza Zanzibar, JUMAZA inatoa tamko lifuatalo:-
JUMAZA inawatanabahisha wananchi wote kuwa Taasisi za kiislamu Zanzibar
kamwe hazihusiani na vurugu hizo kwani zenyewe zinapigania amani,
utulivu mshikamano umoja na udugu kama inavyoelekezwa katika Dini yetu
tukufu ya Kiislamu.
JUMAZA inalaani vikali wale wote waliofanya fujo na hujuma zilizopelekea
maafa katika nchi yetu kwa kutumia kichaka cha “ Kutekwa Sheikh Farid
Hadi”.
Comments