Skip to main content

TASWA YALAANI MASHABIKI WA MOTEMA PEMBE KUMDHALILISHA MWANDISHI WA JAMBO LEO.

CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimesikitishwa na kinalaani tukio lililomkumba mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la JamboLeo, Asha Kigundula wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Simba na DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jumapili iliyopita.
Mwandishi huyo pamoja na Watanzania wengine waliokuwa Kinshasa, DRC kushuhudia mchezo wa Simba na DC Motema Pembe kwenye Uwanja wa Mashujaa ‘Stade des Martyrs’ walifanyiwa fujo ambazo hatukutarajia kama mashabiki wenye busara wangeweza kuzifanya. Kilichotusikitisha zaidi ni hatua ya mashabiki hao kumdhalilisha mwandishi huyo bila kujali utu wake, heshima yake na thamani yake, kisa tu ni Mtanzania ambaye alikuwa uwanjani hapo kushuhudia timu ya Tanzania ikicheza. Kamati ya Utendaji ya TASWA itakutana haraka iwezekanavyo kuhusiana na tukio hili ili kupata maelezo ya kina kwa vile Katibu Mkuu wa chama, Amir Mhando alikuwepo Kinshasa katika mchezo huo , hivyo atakuwa msaada mkubwa kueleza namna ya mambo yalivyokuwa. Baada ya hapo TASWA itaangalia hatua ambazo kama chama na waandishi wa habari za michezo kwa jumla wanaweza kuchukua kwa jambo hili, kwani hata waandishi wa habari za michezo wa DRC, hawakutoa ushirikiano kwa wenzao wa hapa kama ambavyo wao walipewa wakati walipokuja Dar es Salaam na timu yao.
Kwa sasa Sekretarieti ya TASWA inafanya mawasiliano na Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Rage pamoja na Asha kuhusiana na namna bora ya kuchukua hatua za kisheria kwa jambo hili.
Tayari Rage amesema hatua ya awali atamjulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuhusiana na kudhalilishwa kwa mwandishi huyo na vurugu nyingine ambazo Simba ilifanyiwa Kinshasa na baada ya hapo tutaona hatua gani nyingine zifuatwe.
TASWA inaamini kama mashabiki wa DC Motema Pembe wangetumia kauli mbiu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayosisitiza amani michezoni 'Fair Play', hakika baadhi ya mambo yasingejitokeza. Watanzania ni watu waungwana sana, tumekuwa mara kwa mara tukifanya hivyo kwa wageni wetu, hatutaki kulazimika kuharibu sifa yetu nzuri, hivyo tunaamini mamlaka husika zitafuatilia jambo hili kwa umakini zaidi.Chanzo ni www.fullshangwe.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...