Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na baadhi ya marais wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika AU wakimpongeza Rais mstaafu wa Brazil Lula Da Silva kwa hotuba yake aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Wakuu wa nchi za AU uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sipopo,jijini Malabo,Equatorial Guinea jana asubuhi.Hotuba hiyo ya kusisimua ilitilia mkazo kwa nchi za Afrika kushirikiana ili kujiletea maendeleo na kuepuka misaada yenye masharti inayolididimiza bara la Afrika katika lindi la umaskini.
Rais Jakaya Kikwete akishiriki kupanda mti wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano wa Wakuu wa Umoja wa Afrika(AU) katika mji mkuu wa Guinea ya Ikweta, Malabo.|
Comments