Bw Lavrov anasema hatua hio ikiwa imedhibitshwa ni kosa kubwa kwani imekiuka azimio 1970 la umoja wa mataifa ambalo linazuia silaha kuingizwa nchini humo na pande zote husika kwenye mzozo huo.
Wanjeshi wa Ufaransa walikiri kuwaangushia silaha wapiganaji wa kabila la Berber wanaoishi kwenye maeneo ya milima kusini mwa mji mkuu wa Tripoli.
Umoja wa Afrika pia umelaani uaamuzi wa Ufaransa wa kuimarisha nguvu za kijeshi za waasi hao.
Mwenyekiti wa tume ya Umoja huo Jean Ping amesema kitendo hicho kinaweka eneo zima hatarini.
Waziri wa mambo ya nje wa urusi amepanga kukutana na mwenzake kutoka Ufaransa Alain Juppe mjini Moscow kudhibitisha suala hilo tete.
Serikali ya urusi ilisusia kupigia kura mswada uliowasilishwa kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa kuruhusu harakati za kijeshi nchini Libya.
Mzozo unaoendelea mjini Libya ndio umepewa kipa umbele katika mkutano wa viongozi wa Afrika unaoendelea nchini Equatorial Guinea.
Bw Ping amesema kuna uwezekano mkubwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vikazuka nchini humo sawa na hali iliyoko nchini Somalia.
Mwenyekiti wa tume hiyo ya Umoja wa Afrika amefahamisha BBC kuwa mpango wa amani uliyobuniwa mnamo mwezi March bado unazingatiwa.
Mpango huo unataka pande zote zisitishe mapigano ili mazungumzo ya amani yaweze kuanza.
Habari kwamba Ufaransa imedondosha silaha nchini Libya zilijitokeza kupitia gazeti la Ufaransa, Le Figaro la jumatano.
Gazeti hilo lilisema kuwa Ufaransa, nchi inayoongoza operesheni ya NATO nchini Libya haikufahamisha nchi wanachama wenzake kuhusu operesheni hio.
Chanzo ni bbckiswahili
Comments