Fidelis Butahe, Igunga
MJI wa Igunga na vitongoji vyake jana ulizizima, Mbunge wa Igunga Rostam Aziz alipotangaza kuachia ubunge wa jimbo hilo.Tukio hilo liliambatana na matukio kadhaa ya wananchi kuonyesha mabango yaliyokuwa na ujumbe tofauti, wengine kuzirai na mara kadhaa kumvamia ili asiendelee na uamuzi wake huo.
Mbunge huyo aliwasili Igunga saa saba mchana na baada ya kufika akaingia katika ofisi za CCM wilaya na kuzungumza na Baraza la Vijana la Wilaya. Aliwambia vijana hao kwamba, halikuwa lengo lake kuingilia mkutano wao bali alitaka kuzungumza na wazee.
Wakati akiingia katika mkutano huo, alipokewa na mabango yaliyokuwa na ujumbe uliosomeka kwamba "Kama wakikufukuza na sisi tutaondoka CCM”, “Igunga bila Rostam hakuna maendeleo”, “Rostam umeboresha huduma za kijamii Igunga”, “Mbunge wetu tunakupenda sana” na “Tuna imani na wewe”.
Alitumia dakika saba kuzungumza na vijana kabla ya kukutana na viongozi wa CCM wa wilaya hiyo, akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee, Kassim Ally. Akiwa na viongozi hao alizungumza nao kwa dakika 49.
Saa nane mchana aliondoka kwenda kwenye Ukumbi wa Sakao uliopo kilomita moja kutoka jengo la CCM wilaya hiyo.
Akiwa huko alipokewa na kisha kuanza kusoma hotuba yake ndefu ya kurasa takribani 10, lakini mara baada ya kutangaza kuachia nafasi zake ndani ya CCM huku akilengwa na machozi, baadhi ya wanachama walianza kulia huku wengine wakivamia meza kuu kumtaka mbunge huyo abadili uamuzi yake.
Wananchi hao walikuwa wamebeba mabango yenye maneno “ wao CCJ, sisi CCM”, huku wakilitaja jina la Nape Nnauye, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho.
Kufuatia tukio hilo Rostam alilazimika kuacha kuendelea kuisoma hotuba hiyo kwa dakika 15 baada ya kuvamiwa na kundi la baadhi ya vijana waliomtaka kusitisha uamuzi wake huo na kuwasihi wasimzuie, ili amalizie hotuba hiyo na baadaye watoe maoni yao.
Baada ya wanachama hao kutulia walipewa nafasi ya kutoa maoni yao wakasema kwamba akiendelea na uamuzi huo watarudisha kadi za CCM.
"Hatukubali wewe kwetu ni muhimu sana umetufanyia mengi, yanayosemwa yavumulie nakuomba ubadili msimamo wako na kama hautabadili msimamo huo hatuoni haja wa kubakia ndani ya chama cha CCM," alisema Hamis Kanama.
Watu wazirai
Baada ya Rostam kumaliza kusoma hotuba, Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nzega, Daudi Ngutu, na Katibu wa Uchumi Kata ya Igoweko, Athuman Kanyama, walizirai na kupandishwa katika gari la Halmashauri ya kupelekwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya.
Mjumbe wa Barala la Utekelezaji la UVCCM, Hussein Bashe, alikuwa miongoni mwa mashuhuda wa tukio la Rostam kutangaza kung’atuka. Bashe ambaye alikuwa sambamba na Rostam tangu akiwa katika ofisi za wilaya aliliambia Mwananchi kuwa uamuzi wa Rostam ni mwiba mchungu kwa wananchi wa jimo hilo.
"Alichokifanya Rostam ni haki yake, lakini pamoja na hayo hawatendei haki wananchi wa Igunga, ila kwa kuwa ni maamuzi yake hakuna jinsi,"alisema Bashe na kusisitiza kwamba, CCM isipokuwa makini uchaguzi wa mwaka 2015 ukimalizika, utakiacha kikiwa chama cha upinzani na si chama tawala.
"Sekretarieti ya CCM itakabidhi chama kikiwa cha upinzani Watanzania wana matatizo mengi , lakini viongozi badala ya kuangalia hayo wanaendekeza siasa za chuki na kinafiki," alisema Bashe.
Rostam aondolewa na mabaunsa
Wanachama wa CCM waligoma kumruhusu Rostam kutoka katika ukumbi huo mpaka abadili uamuzi wake hali iliyosababisha vurugu na kufanya Askari wa kutuliza Ghasia(FFU) kuingilia kati.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa CCM walimtoa Rostam katika ukumbi huo kwa kuwatumia mabaunsa waliokuwa wanawazuia wananchi wasimzuie Rostam kuondoka.
Wakati Rostam akiwa njiani kuondoka kwenda Dar es Salaam wanachama wengine ambao ni Katibu mwenezi kata ya Chabutwa, Athumani Mihayo, Catherine Mabula na Zainabu Athumani walizirai.
Viongozi wa CCM waliokuwapo
Viongozi wa CCM wengi kutoka wilaya zote za mkoa wa Tabora walihudhuria ambao ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga, Katibu Tawala wa Wilaya, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tabora, wajumbe wa kamati ya siasa wa wilaya na Baraza la Wazee la Wilaya na Mbunge wa Viti Maalumu, Munde Tambwe.
Chanzo: Mwananchi.

Comments