POLISI KANDA MAALUM YA DAR YATHIBITISHA KUMKAMATA MWANAFUNZI ALIYESAMBAZA PICHA ZA KUWEPO KWA NYUMFA JENDO UDSM
picha milladayo
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limetoa taarifa ya kukamatwa na kuachiwa kwa Mwanachuo wa Chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM baada ya kusambaza picha kwenye mitandao ya kijamii zinazoonyesha Hostel mpya za wanafunzi zikiwa na ufa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amezungumza na wanahabari ambapo amethibitsha kuwa wamemkamata na kumwachia mwanafunzi huo baada ya kubainika amesambaza picha hizo kwenye mitandao.
Kamanda Mambosasa amesema mwanafunzi huyo amefanya uzushi wa kusambaza taarifa hizo jambo ambalo waliopaswa kutoa taarifa ya majengo ni wamiliki wa majengo.
Hata hivyo Kamanda Mambosasa amesema Polisi ilimkamata na kumuhoji mwanafunzi huyo kwa lengo la kujua hasa la yeye kusambaza picha hizo pasipo kutoa taarifa kwa wamiliki wa majengo
Comments