Shirika la damu salama Tanzania limejipanga kufanya kampeni ya uchangiaji damu nchi nzima ili kutoa msaada kwa wagonjwa wanao hitaji msaada wa damu kwa nchi nzima.
Afisa uhusiano wa mpango wa Taifa wa Damu Salama Rajabu Mwenda amesema kuwa wanatarajia kuanzisha kampeni ya kukusanya damu nchi nzima kwa kushirikiana na halmashauri na hospitali za rufaa kama KCMC,Bungando,Muhimbili,mbeya na JKCI.
Aidha Mwenda amebainisha kuwa kampeni hiyo inatarajiwa kuanza rasmi Disemba 11 na kumalizika disemba 15 amesema lengo la kampeni hiyo ni kutoa elimu na kuongeza makusanyo ya damu kwa mwaka 2017.
Aidha ametoa wito kwa wanachi kujitokeza katika vituo vya kutoa damu vya mpango wa damu salama na sehemu yoyote ambapo zinatolewa huduma hizo.
Comments