Baraka The Prince amefunguka amechoshwa na mtu ambaye anamfanyia hujuma katika mtandao wake wa 'Youtube'
Baraka The Prince amefunguka na kusema kuwa amechoshwa na mtu ambaye anamfanyia hujuma katika mtandao wake wa 'Youtube' na kuamua kutangaza dau la milioni tatu kwa mtu ambaye anaweza kumgundua mtu ambaye anapunguza watazamaji wake kwenye mtandao huo.
Baraka awali alikuwa akilalamika akionyesha kuwa mtu ambaye anamfanyia hujuma hizi anamtambua kuwa ni moja kati ya viongozi wake ambao walikuwa wakimsimamia katika kazi zake za muziki.
"Kwanza nishukuru sana mashabiki zangu mnaojitahidi kunipigania na kupoteza muda wenu kwa ajili ya kazi lakini kuna mtu mmoja tu ambae aliumbwa kurudisha nyuma hatua za watu. Kila siku 'viwes' wanazidi kupungua sasa basi natangaza kumpa zawadi ya Tsh Milioni 3 kwa yeyote atakayetuthibitishia na kutuletea uyu mtu" aliandika Baraka The Prince
Aidha Baraka aliendelea kulalamika "Maana huku ni kudharau kazi yangu na kudharau muda wa mashabiki zangu, Radio na Tv na vyombo vyote vya habari ambavyo vimenipigania takribani miaka 5 sasa nikiwa katika tasnia ya bongo fleva"
Comments