CHAMA cha Wananchi CUF kwa upande wa wanaongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba kimechukizwa na hatua kukihama na kujiuzulu ubunge wa jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia .
Mkurugeni wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa CUF, Abdul Kambaya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Hayo yamesemwa mble ya waandishi wa habari leo Dar es Salaam na Mkurugeni wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa CUF, Abdul Kambaya amesema kutokana na kitendo hicho kimeomba radhi wapiga kura wa jimbo hilo.
" CUF kinachukua fursa hii kuwaomba radhi wapiga kura wa jimbo la Kinondoni kwa kuwaaminisha Maulid Said Abdallah Mtulia ni mtu makini anaweza kusimamia sera za chama na maendeleo ya wanakinondoni kwa ujumla wake," amesema.
Akizungumzia kuhusu sababu zilizomfanya Mtulia kujiunga na CCM amesema hazina mashiko.
"Kuunga mkono jitihada za rais katika kurekebisha uchumi na mambo mbalimbali sio lazima kujiondoa uanachama. Lakini hapa suala la kujiuliza ni kwamba Mtulia anamuunga mkono rais Magufuli au anaunga mkono CCM? maana kuna baadhi ya wanaccm wanapinga jitihada zinazofanywa na rais katika suala la usimamiaji wa rasilimali ". amehoji na kusema.
Kambaya amesema uamuzi wa kujiondoa kwenye chama ni utashi wake ambao hawadhani kama kuna ushawishi toka upande wa Serikali au CCM uliopelekea Mtulia kujivua uanachama.
Amesema watasimamisha mgombea mwingine katika jimbo hilo na kuwataka wapenzi na wanachama kuwa watulivu.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments