BONDIA Idd Pialali amehadi kuibuka na ushindi katika pambono lake
lake litakalo fanyika kesho dhidi ya mpinzani wake kutoka India aitwaye
Shiva litakalokuwa la raundi 10 lenye uzito wa Kg 66.6 lenye kutambuliwa
kimaitaifa(U.B.O).
Kuelekea pambano hilo Mratibu wa pambano hilo Sharifu Mkusini kutoka katika kampuni ya
Sharifu Promoterameuambia mtandao huu kuwa mabondia hao wamepima uzito leo(Jana) mjini
Bagamoyo Mkoani Pwani katika ukumbi wa Traveler Lodge mjini humo.
Alisema kutakuwa na mapambano mengine katika kuhusindikiza mpambano wa huo,
ambapo bondia Dulla Mbabe atapanda kuzipiga na George Pimoso
,huku mambondia wengine wakitajwa kuwa ni Bruno Vifua viwili ambaye atazichapa
na Saidi Uwigo katika,Rehema Nakozi akipanda kuzichapa na Happy Daudi katika
mapambano ya takayokuwa ya raundi 8.
"Tumeandaa pambano hili kwa kumleta bondia wa India kwakuwa tunataka wapambane
kuleta sifa zaidi nchini kwani mara kwa mara mabondia wetu wamekuwa na sifa
ya kupigwa na mabondia kutoka India,"alisema Sharifu.
Alisema katika pambono hilo amewaomba wakazi wa Bagamoyo kujitokeza kwa wingi
kwani mpambano huo utakuwa wakipekee sana huku bondia Idd akiwa ameahidi kuwapa
raha watanzania.
"Nitawapa raha kwa kumchapa katika dakika ya 3 bondia huyo kutoka India kwani
malengo yangu ni kupata ushindi wa mapema sana ilikuwapa furaha watakao fika
katika ukumbi huo,"alisema Idd.
sHARIFU Promotar imetaja kiingilio katika pambano hilo litakalo anza saa 12:00
usiku siku ya Jumamosi kuwa VIP kiingilio kitakuwa Sh 15,000 huku maeneo
mengine yakitajwa kuwa ni Sh.1000 tu kwa kila mmoja ambapo wadhamini wametajwa
kuwa ni Traveler Lodge , Kinite Castle pamoja na New Africa Casino.
Comments