KOCHA wa timu ya Everton, Sam Allardyce amemuweka staa wa Watford Striker Troy Deeney mwenye miaka 29 kuwa chaguo lake la kwanza baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa.
Allardyce pia amesema kwamba atahakikisha kiungo Ross Barkley anasalia katika kikosi chake.
Big Sam anafahamika kwa vurugu zake wakati wa usajili na mara yake ya mwisho aliondoka timu ya taifa ya England kwa kashfa baada ya kampuni ya Asia kumtumia kama njia ya kunasa mastaa wa Ulaya.
Comments