Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga akizungumza na wahitimu wa chuo cha Utalii
Viongozi wa chuo Cha Taifa cha Utalii aliyekaa wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Taifa cha Utalii ndg Stephen Madenge.
baadhi ya wanafunzi waliohitimu mafunzo Chuo cha Taifa Cha Utalii
wanafunzi waliohitimu Chuo Cha Taifa Cha Utalii
Mkufunzi wa Utalii Robert Leshinga akipambanua jambo mbele ya wanahabari.

JUMLA ya wanafunzi 129 wa Chuo cha taifa cha Utalii wamehitimu jana mafunzo ya taaluma ya Utalii ambapo wametakiwa kwenda kutumia ujuzi na ueledi wa mafunzo waliyoyapata chuoni hapo.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga ametoa wito huo leo wakati akizungumza na wanafuzi wa chuo hicho katika mahafali ya 15 kwa ngazi ya stashahada na astashahada ambayo yamefanyika jijini Dar es salaam .
Kwa upande wa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Utalii DK.Shogo Mlozi Sedoyeka amesema licha ya kuwepo na changamoto mbalimbali wamejipanga kuweza kuzitatua ili kuendelea kuboresha elimu bora kwa wanafunzi.
Mmoja wa wahitimu hao Deogratius Tarimo amesema watanzania wengi wamejijengea kuwa dhana ya utalii inawahusi wageni kutoka nje ya nchi na kuwa mchakato wa kufanya utalii wa ndani wazawa wanapaswa kutembelea mbuga za wanya kwa kufanya hivyo watapata kuzitazama fursa zilizopo nchini.
Katika Mahafali hayo yalio hudhuria na wahitimu kutoka(campas) za Chuo cha Utalii kilichopo Temeke na Arusha ambapo vijana waliohitimu wamekuwa wakipata utashi zaidi ilikuweza kupata nafasi ya kuajiria katika maeneo mbalimbali.
Chuo hicho Cha Taifa cha Utalii kwa sasa imeelezwa kimeingia makubaliano na Chuo kikuu cha Vancuva ili kujifunza mbinu mbalimbali za kutoa mafunzo bora kwa wanafunzi.
Comments