Licha ya kuundwa na safu kali ya ushambuliaji, timu ya Paris Saint German ya Ufaransa imefundishwa soka na miamba ya Ujerumani, Bayern Munich.
PSG ikicheza ugenini kwenye dimba la Allianz Arena, ikakubali kichapo cha bao 3-1 kwenye mchezo mkali wa Ligi ya Mabingwa.
Si Cavani wala Neymar waliofanikiwa kupeleka madhara kwenye lango la Bayer Munich na badala yake ni mshambuliaji kinda Kylian Mbappe ndiye aliyefanikiwa kuipatia PSG bao pekee kunako dakika ya 50.
Robert Lewandowski aliifungia Bayer Munich bao la kwanza dakika ya 8, kabla Corentin Tolisso hajawafungia wenyeji goli la pili dakika ya 37 na la tatu katika dakika ya 69.
Pamoja na kipigo hicho, PSG imefanikiwa kuibuka kinara wa kundi B kwa kujikusanyia pointi 15 sawa na Bayer Munich iliyoshika nafasi ya pili, lakini PSG wanabebwa na utajiri wa wastani mzuri wa magoli.
Comments