Serikali imesema shule za taasisi za kidini zimepoteza mwelekeo kwa kuwa zimeanza kuzalisha vijana wa vijiweni na baadhi zinatajwa katika suala la ushoga.
Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Maria Semakafu wakati akifungua mkutano wa umoja wa shule za seminari na binafsi uliofanyika mjini hapa.
Dk Semakafu alikemea tabia ya ushoga kuwa imeanza kuota mizizi kwani vijana wengi wa mitaani wakiulizwa mambo ya ushoga walijifunzia wapi wanazitaja shule za dini.
"Haya siyo maadili mliyokuwa mkifundisha tangu awali, kafundishe maadili ya kidini kama mlivyokuwa awali, tunapata malalamiko mengi kutoka kwa wazazi na wanafunzi wanaosoma huko kuhusu tabia hizo chafu," amesema Semakafu.
Amesema kwa sasa shule hizo zimekuwa na maadili mabovu akaagiza warekebisha mienendo yao haraka kwani Serikali haitavumilia vitendo hivyo.
Comments