Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Fortunatus Musilimu(picha na mtandao)
Katika Kuelekea mwisho wa mwaka 2017 Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani limetoa twakimu za sikukuu ya krismas ya mwaka huu zikionyesha kumetokea jumla ya ajali 10 zilizosababisha vifo 5 na majeruhi 11 zikilinganishwa na takwimu za mwaka jana za krismas.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salama Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Fortunatus Musilimu amesema kutokana na takwimu hizo amewatoa hofu watanzania wanaotumia barabara na kuwahakikishia kuwa kupitia operesheni ya KA-MA-TA itasaidia kupunguza ajali barabarani.
Musilimu amesema kuwa wamejipanga kweli kweli kuwadhibiti madereva wazembe na wamejitahidi kupunguza ajali huku akitolea mfano siku ya leo kuwa zimetokea ajali 3 tu.
Pia amewahakikishia watu wote wanaosafiri katika kipindi hiki cha sikukuu kuwa watasafiri salama bila tatizo lolote huku akiwataka madereva wanaoendesha vyombo vya moto kutii sheria bila ya shuruti.
Hata hivyo Kamanda amesema watawachukulia hatua kali za kisheria madereva wote wasiotaka kubadilika kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali zinazoweza kujitokeza zinazosababishwa na uzembe wa madereva.
Comments