Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza kuingia mkataba mkataba wa miaka miwili na kampuni ya vifaa vya michezo ya Macron.
Kwenye mkataba huo Macron itakuwa ikitengeneza jezi kwa ajili ya timu ya wakubwa, Taifa Stars na zile za wanawake pamoja na vijana.
Akitaja kiasi cha fedha walichopata kwenye mkataba huo, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema mkataba huo utagharimu kitita cha Tsh milioni 800 kwa miaka hiyo miwili.
Karia amesema kampuni hiyo itakuwa ikiwatengenezea vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo jezi za timu za mpira wa miguu za taifa.
Comments