KLABU ya Liverpool inaendelea kuota kuinasa saini ya staa wa Southampton Van Dijk raia wa Uholanzi ambaye walimkosa katika dirisha lililopita.
Staa huyo pia alikuwa alikuwa akiwindwa na klabu ya Chelsea ambayo pia imepanga kurudi mezani mwezi Januari.
Wakati huohuo klabu za Manchester United na Juventus zinaendelea kupigana vikumbo kuwania saini ya kiungo wa timu ya Monaco, Fabinho mwenye miaka 24.
Comments