Ramsey Nouh alipokwenda kutembelea kaburi alilozikwa Marehemu Stephen Kanumba
Ramsey akiwa amekumbatiana na Mama Kanumba
Muigizaji maarufu kutoka nchini Nigeria Ramsey Nouh ametua nchini wiki Tanzania kwa lengo la kukutana na wanasini wa filamu nchini.
Ramsey Nouh ambaye alifanya moja ya filamu iitwayo “King Of Devil”ambayo alishirikiana na aliyekuwa msanii nyota wa filamu nchini Tanzania Marehemu Stephen Kanumba ambapo jana alichukua jukumu la kwenda kutembelea kabuli alilozikwa marehemu Kanumba.
“Steven, kwa mara ya mwisho tulizungumza sote tukiwa hai lakini leo nimesimama kando yako ukiwa umelala chini ya mchanga hujitambui, kwangu ni zaidi ya msiba na kwa kweli nimeshindwa kuhimili jambo hili, najua huko uliko unaumia sana hususan ukizingatia ukweli kwamba tasnia ya filamu za Kitanzania inakufa,” alisema Ramsey katika mazungumzo yale na Kanumba
Comments