Sadick Japhari, mkazi wa Tabora amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kufanya mapenzi na binti yake mwenye umri wa miaka 16 hatimae kumsababishia ujauzito na kukatisha masomo yake akiwa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Lwanzari Tabora mjini.
Mtuhumiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora na kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena shauri lake namba 49 la mwaka 2017 likiwa upande wa kutolea ushahidi kwa upande wa Jamhuri ambapo ilikuwa ni zamu ya kutoa ushahidi kwa Afisa mtendaji wa mtaa wa shule Kata ya Kaloleni, Christina Kitundu kuwasilisha ushahidi wake ambapo alieleza Mahakama kwamba mtuhumiwa Sadick ambaye alikuwa akiishi na binti yake katika nyumba yenye chumba kimoja na sebule alikuwa akifanya tendo la ndoa wakati binti yake akiwa amelala.
Christina ameiambia mahakama mbele ya mahakama Mkazi Mfawidhi wilaya ya Tabora mjini Jaktoni Lushwela kwamba mtuhumiwa baada ya kubaini tayari amekwisha msababishia binti yake ujauzito aliamua kumasfirisha ikiwa ni mpango wa kuficha ukweli.
Hata hivyo kwa kuwa Afisa Mtendaji wa mtaa ambaye alikuwa na jukumu la kufuatilia watoto wanaoacha masomo kwasababu mbalimbali akuchukua hatua ya kumrejesha Tabora binti huyo na hapo ndipo alipojiridhisha kuwa ni mjamzito na siku chache baadae akajifungua mtoto wa kiume.
Aidha mtoto huyo aliieleza Mahakama kuwa baba yake huyo amekuwa akimbaka mara kadhaa majira ya usiku tangu mwezi Januari 2017 wakati akiwa nyumbani huku akimtia kumdhuru endapo jambo hilo atalisema mbele za watu.
Mtuhumiwa huyo aliukana ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa daktari Disemba 19 mwaka huu, huku mtuhumiwa akiendelea kusota rumande.
Comments