Mtalii kutoka Ujerumani auawa kwa kupigwa risasi Ethiopia Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako
Mtalii mmoja kutoka Ujerumani amepigwa risasi na kuuawa kaskazini mashariki mwa Ethiopia.
Dereva wake pia alijeruhiwa wakati wa tukio hilo, ambalo lilifanyika katika jimbo la Afar, karibu na mpaka wa Eritrea.
Ripoti zanasema raia huyo wa Ujerumani alikuwa miongoni mwa kundi la watalii ambao walikuwa kwenye ziara ya volkano ya Erta Ale - kivutio kikubwa kwa watalii wanaozuru Ethiopia.
Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anasema hadi kufikia sasa haijabainika ni nani hasaa aliyetekeleza shambulio hilo lakini serikali ya Ethiopia inasema inachunguza mauaji hayo.
Serikali pia inasema vikosi vya usalama vimetumwa kuimarisha usalama huko.
Eneo hilo la mpakani linatumika sana na kundi la waasi linalotaka kujitenga na Ethiopia.
Mnamo mwaka 2012, watalii watano waliuawa na wengine wanne kutekwa nyara baada ya wapiganaji kuwashambulia katika eneo hilo.
Kundi lililojihami la Afar Revolutionary Front lilidai kuhusika kwenye shambulio hilo.
Comments