Ndugu zangu,
Kwa
mila zetu, kwenye misiba na majanga kama haya watani wana jukumu la
kufariji wafiwa kwa kuingiza utani na watu wakacheka badala ya kulia
muda wote.
Naam, miaka kadhaa iliyopita niliweka hapa picha ya kwanza hapo juu nikiwashangaa watani zetu Yanga kwa kujenga jengo na uwanja bonde la Msimbazi. Leo tumeona ukuta wa uwanja umevunjika na jengo lenyewe la klabu liko hatarini kama gharika itarudi tena.

Hivi
wazee wa Yanga wa enzi hizo walishindwa kupata kiwanja katikati ya mji?
Walishindwa kupaa eneo la kujenga uwanja wa maana pasipo bondeni? Oneni
jengo la Simba hapo Msimbazi Street! Dar kutafurika kote lakini si
Msimbazi Street! Mtaa maarufu kuliko yote na wenye jengo la klabu
maarufu kuliko zote!
Ndugu zangu na watani zangu Yanga,
Utani huu hauna mahusiano na picha ya chini kabisa nikiwa na kaka yangu Issa Michuzi, hata kama na yeye ni Yanga dam dam!
Maggid,
Iringa. Toka kwa Maggid mjengwa.
Comments