Mkurugenzi
wa masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Ephraim Mafuru
akizungumza katika uzinduzi wa bia mpya ya Senetor Extra Lager ambayo
imeanza kuzaliashwa na kusambazwa na kampuni hiyo. Bia hiyo inawalenga
wachapakazi wa hali ya chini kabisa, wakulima, wavuvi na wengineo wa
kanda ya ziwa na majirani zake. Bia ya Senetor itauzwa kwa bei nzuri ya
shilingi elfu moja na mia tatu tu (1,300/-)
Na Mashaka Baltazar,MWANZA
KAMPUNI
ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kinywaji kipya cha bia ya
Senator, kinachozalishwa kwa kutokana na mazao ya mtama na shayiri na
kuwataka wakulima wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kulima mazao hayo kwa vile
watakuwa na soko la uhakika. Hafla
ya uzinduzi huo ilifanyika jana katika kiwanda cha SBL
Mwanza,kuhudhuruiwa na baadhi ya wafanyakazi,mawakala na wauzaji wa
bidhaa za kampuni ya SBL. Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kinywaji hicho kipya,
Mkurugenzi wa Masoko wa (SBL) Ephraim Mafuru,alisema serikali
inawaunga mkono kwa kusisitiza wakulima kuchangamkia kilimo cha mazao
ya mtama na shayiri. Alisema
kuwa wakulima wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wanapaswa kuanzisha kilimo
cha mtama na kuuza mazao yao katika kiwanda cha SBL kinachozalisha
kinywaji hicho na watakuwa na soko la uhakika.
“Tunaagiza
malighafi kutoka nje ya nchi kwa asilimia 80 ili kukidhi mahitaji kwa
sababu asilimia 20 ya malighafi ya hapa nchini ni ndogo,hivyo
wakulima wa Kanda ya Ziwa wanapaswa kulima na kuuza mazao yao
kiwandani kwetu na wao kunywa kinywaji hiki cha Semator ili kusukuma
biashara hii.
Soko la mazao yao kama mtamama na mahindi linapatikana
SBL ambapo tumekuwa tukinunua kilo moja ya mtama kwa shilingi
600,”alisema Mafuru alisema
kuwa bia ya Senator yenye kilevi cha asilimia 6 inazalishwa kutokana
na kimea cheupe kinachotokana na mtama, kinywaji ambacho kimemlenga
mtanzania wa kipato cha kawaida wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Alieleza
kuwa kinywaji hicho tayari kipo sokoni na kuwataka wateja wake ambao
ni wavuvi na wakulima kukinunua ambapo bei ya mlaji itakuwa ni
shilingi 1300,ambapo Januari mwakani watafanya matamasha ya
kukitangaza kinywaji hicho zaidi katika maeneo ya vijijini.
Aidha
alisema kauli mbiu ya kinywaji hicho ni ‘bia ya wachapakazi ahsante
kwa kutuwezesha kuwa kampuni kubwa’ ambapo SBL inatarajia kudhamini
ngoma za utamaduni za makabila ya Wasukuma za Wagika na Wagalu. Kwa
upande wake Meneja Mauzo wa SBL Kanda ya Ziwa, Stansaus Theophile,
alisema bei tishari moja ilenye chupa 25 liytauzwa kwa bei ya shilingi
25 kwa mawakala,shilingi 25,400 (mawakala wa kati) na shilingi
26,000 kwa mawakala wadogo na mlaji shilingi 1300.
Comments