Skip to main content

Maalim Seif: Zanzibar iwe na Benki Kuu; Mafuta na gesi si vya Muungano; Urais wa Muungano kwa Mzunguko

 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema ni muhimu kwa sasa Zanzibar kuwa na benki kuu yake ikiwa inataka kutumia kikamilifu rasilimali zake kujenga uchumi wake.  

 
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, akizungumza katika viwanja vya Kibandamaiti mjini hapa juzi alisema kuendelea kutegemea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kunainyima Zanzibar kutekeleza mipango yake ya maendeleo kwa ufanisi.  

Aliuambia umati mkubwa uliojaa kwenye viwanja hivyo kuwa wananchi visiwani humo wanaweza kudai haki ya Zanzibar kuwa na benki kuu kwa njia ya kutoa maoni kupitia hatua mbalimbali za mchakato unaoendelea juu ya Katiba mpya ya Tanzania.  

Akizungumzia huduma za BoT kwa Zanzibar, Maalim Seif alisema uwiano mbaya wa wafanyakazi kutoka pande mbili za Muungano unasababisha upungufu wa wataalam wa kuishauri benki hiyo juu ya mahitaji ya Zanzibar, “Ikiwa kwa mfano BoT ina wafanyakazi 80 na wanne tu wanatoka Zanzibar, bila shaka uwiano huo ni mbaya katika suala la utoaji vipaumbele kwa maendeleo ya visiwani,” alisema Maalim Seif.  

Alisema umuhimu kwa Zanzibar kuwa na benki kuu yake sio jambo jipya, kwani hata awamu ya kwanza ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliweka wazi madai ya aina hiyo ikitaka kila upande uwe na mambo yake katika masuala ya kibalozi, shughuli za polisi, uraia na sarafu.  

Alisema wakati wa kutoa maoni juu ya Katiba mpya, pamoja na kudai haki ya kuwa na benki kuu, wananchi waungane ili maoni yao yaweze kusaidia upatikanaji wa katiba itakayoondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya muungano.  

Maalim Seif alisema ukosefu wa umoja miongoni mwa wananchi katika suala la kudai maslahi ya Zanzibar ndani ya Katiba mpya ni hatari kwa utaifa wao, “Utakapofika wakati wa kutoa maoni tusahau itikadi zetu, tuungane kulinda maslahi ya Zanzibar, vyama vya siasa ni taasisi za kupita, ASP haipo, TANU haipo na ZNP haipo, lakini Zanzibar itaendelea kuwepo,” alisema.  

Maalim Seif pia alisisitiza msimamo wa kutaka Katiba mpya itakayoundwa iweke utaratibu unaoruhusu mzunguko wa madaraka ya nafasi ya rais wa muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika, “Mwandishi mmoja wa habari juzi alitaka nieleze maslahi ya Zanzibar ninayowahimiza wananchi kudai yawekwe ndani ya Katiba mpya, nikamwambia mfumo wa sasa wa uchaguzi umesbabisha nafasi ya rais wa muungano kubaki bara kwa muda mrefu,” alisema Maalim Seif akiwa anarejea jibu alilotoa katika mkutano wake na waandishi wa habari baaya kuulizwa swali hilo na Muhibu Said, Mwandishi wa habari mwandamizi wa NIPASHE.  

Akifafanua zaidi haja ya kuwepo utaratibu wa kikatiba unaoruhusu nafasi hiyo kutolewa kwa mzunguko, Maalim Seif alisema chini ya mfumo wa uchaguzi uliopo Zanzibar imeshika nafasi hiyo kwa miaka 10 tu wakati Tanzania bara imehodhi wadhifa huo kwa miaka 35. 

Alisema hiyo ni kasoro katika uendeshaji wa serikali ya muungano iliyoundwa na mataifa mawili ambayo ni nchi.  Nipashe Jumapili.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...