VIONGOZI NA WANANSIASA WATAKIWA KUEPUKA KUWATETEA WANANCHI WANAOHARIBU MAZINGIRA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hasan akikagua bidhaa za wajasiriamanli mbalimbali kwenye viwanja vya mnazi mmoja
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan(kulia) akiwa anatembea kushoto kwake aliyevaa suti ya blue Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Januari Makamba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan akizindua ukuta maeneo ya barabara ya Barack Obama
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam pamoja na nchi kwa ujumla.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan pamoja na Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Januari Makamba wakitizama ukuta ambao ameuzindua leo.
Baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kwenye uhitimishwaji wa siku ya mazingira.(picha zote na Mussatz)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hasan amewataka viongozi pamoja na wanasiasa kuepuka kuwatetea wananchi wanaojihusisha na uharibifu wa mazingira.
Makamu wa Rais Samia ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam wakati akihitimisha kilele cha siku ya Mazingira iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini hapa.
Aidha Mhe.Samia amesema ni muhimu wananchi wakachukua hatua katika kuhakikisha wanayatunza mazingira na hivyo serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na waharibifu wa mazingira.
Awali akizungumza Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Januari Makamba amesema watahakikisha wanaendeleza jitihada za kuyahifadhi mazingira kwa kuwapa elimu wananchi watumie nishati mbadala na kuepuka mayumizi ya mkaa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye ndiye mwenyeji wa maadhimisho ya mwaka huu kitaifa Paul Makonda amesema wakazi wa Dar es salaam ni wachafu na wanatia aibu hivyo tar 1 july ataanzisha oparesheni ya usafi jijini hapa.
Alvaro Rodrigues ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa akiwa amehudhuria kwenye maadhimisho hayo amesema watahakikisha wanaendelea kufanya kazi kwa pamoja na wananchi wote katika kuyatunza mazingira.
Hata hivyo Mbali na kufanya zoezi la Uhitimishaji wa siku ya Mazingira Mhe Samia amezindua ukuta uliopo barabara ya Barack Obama wenye lengo la kuizuia bahari kuendelea kuimegua ardhi lakini pia kuwa kivutio na kituo muhitu cha mapumziko kwa watu wa Dar es salaam.
Comments