Watu 10 wamefariki
katika ajali iliyotokea baada ya basi la abiria lililogongana na treni
eneo la Gungu katika manispaa ya Kigoma Ujiji, kaskazini magharibi mwa
Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu, ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi na mbili na robo asubuhi.
Basi
hilo la abiria ambalo linamilikiwa na kampuni ya Prince hamida
linadaiwa kugongana na treni lilipokuwa linatoka Kigoma Mjini kwenda
Tabora.
Treni hiyo ya mizigo ilikuwa ikitoka Kazuramimba kwenda Kigoma Mjini.
Rais
wa Tanzania John Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kuwtaaka
„wadau wote wa usalama barabarani kuchukua hatua madhubuti za kuzuia
ajali hizi."
"Vyombo husika, chukueni hatua kali kwa wote wanaokiuka sheria za usalama barabarani," amesema.
- Treni ya starehe ilioundwa India
- Shirika laomba radhi treni kuondoka sekunde 20 mapema
- Kwa Picha: Treni yenye starehe na ghali yaundwa Japan
Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema eneo ilipotokea ajali hiyo hutokea ajali za aina hiyo mara kwa mara.
"Nimezungumza
na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC ) na tumekubaliana
kuwa tuweke kizuizi ( barrier ) Katika eneo hili ambapo reli ikatiza
barabara," amesema.
„ Hii itasaidia sana kupunguza ajali za namna
hii. Mkurugenzi wa TRC Bwana Masanja Kadogosa amekubali ushauri huu
ambao Wananchi wengi wa Kigoma Mjini wamekuwa wakiutoa."Source BBC Swahili.
Comments