Benki ya
Exim nchini imefanya hafla fupi ya futuru (Iftar) pamoja na wateja wake huku ikibainisha
iko katika mchakato kupunguza riba ili kuwawezesha wateja kunufaika na mikopo
na huduma nyingine zitolewazo na benki
hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim,Selemani Ponda akizungumza na waandishi wa habari.
baada ya tafrija fupi ya Iftar iliyoandaliwa na benki hiyo jana usiku Dar es Salaam.
baada ya tafrija fupi ya Iftar iliyoandaliwa na benki hiyo jana usiku Dar es Salaam.
Hatua hiyo
imekuja hivi karibuni baada ya tamko la Serikali kupitia Waziri wa Fedha na
Mipanga, Philip Mipango lililoyataka taasisi za kibenki kupunguza riba za
mikopo kwa wateja ili waweze kunufaika.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim,
Selemani Ponda wakati wa hafla hiyo iliyowakutanisha wafanyakazi na wateja wa
benki hiyo.
Amesema
benki hiyo huwa na utaratibu na kukutana na wateja wake katika Kipindi cha
Mwezi Mtukufu wa Ramdhani na kwamba tayari imeshafanya hivyo katika mikoa
mingine ikiwemo Tanga, Mwanza na Mtwara.
Wafanyakazi wa Benki ya Exim pamoja na wateja wao wakifuturu katika tafrija hiyo.
“ Tumekutana na wateja wetu katika tafrija fupi ya Iftra mwezi huu wa ramdhan hatufanyi hapa hata mikoa mingine tumeshajumuika na wateja wetu nia ni kuwa nao karibu,” amesema.
“ Tumekutana na wateja wetu katika tafrija fupi ya Iftra mwezi huu wa ramdhan hatufanyi hapa hata mikoa mingine tumeshajumuika na wateja wetu nia ni kuwa nao karibu,” amesema.
Amebainisha
kuwa tamko la Serikali la kuzitaka taasisi za kifedha kupunguza riba
wamelisikia na mchakato wa kulifanyia unaendelea na kwamba wakati utakapofika
riba zitawekwa wazi kwa wateja wao.
Amesisitiza
kuwa benki inaamini bado inaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake huku
akiongeza kupunguzwa kwa riba ni njia mojawapo ya kuwanufaisha kwa kuwapatia
riba nafuu.
Kwa upande
wake, mteja wa benki hiyo, Moustafa Khatan ameziomba benki kutoa riba
nafuu na kuajiri wazawa kwa usawa katika
nafasi mbalimbali.
Naye
Mwanzilishi wa Chama cha Watoa Huduma ya Oil na Gesi nchini(ATOGS) ambaye pia
ni mteja wa benki hiyo, Abdulsamad Abdulrahim ameipongeza benki ya Exim kwa
kuwakutanisha na kuiomba iendelee kutoa huduma bora.
Comments