Rais Dk.
John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
Uzinduzi wa
Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo
Awamu ya Pili (ASDP 11) utakaofanyika jijini Dar es Salaam Juni 4 mwaka
huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.k Nyerere.
Waziri wa Kilimo Dkt.Charles Tizeba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Uzinduzi wa ASDP 11wa awamu ya pili utakaofanyika jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo
utahusisha Wizara za kisekta ikiwemo Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Viwanda , Biashara na Uwekezaji na Wizara ya
Maji na Umwagiliaji.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba
wakati akizingumza na wanahabari kuhusiana na uzindunzi wa programu hiyo.
Amesema
shughuli za uzinduzi zitaanza saa 2:00 asubuhi na kwamba progamu hiyo
itatekelezwa katika mikoa na wilaya zote
kwa kuzingatia mazao ya kipaumbele na ikolojia ya kilimo ya kanda 10 kwa
vipindi viwili vya miaka mitano ambapo kipindi cha kwanza kitaanza 2018/19 hadi 2023/24.
Amebainisha
kuwa lengo la ASPDP ni kuleta mageuzi
katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji tija kwenye kilimo, mifugo na
uvuvi, kuongeza pato la taifa la wakulima, wafugaji na wavui pamoja na pato la
taifa kuwa na uhakika wa usalama wa
chakula na lishe.
Amesisitiza
kuwa program hiyo itatekeleza sera mbalimbali ikiwemo Sera ya kilimo ya Taifa,
mifugo, uvuvi, masoko ya mazao ya kilimo, umwagiliaji ya taifa, usalama wa
chakula na lishe, ugatuaji madaraka, maendeleo ya ushirika na Sera ya
mashirikiano kati ya sekta za umma na sekta binafsi.
Amefafanua
kuwa washiriki ni wadau sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi ushirika, wizara,
taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali, washirika wa maendeleo, sekta
binafsi na wananchi kwa ujumla.
Ameongeza
kuwa endapo ASPDP itasimamiwa kikamilifu hadi kufikia mwaka 2020 nchi itafikia
uchumi wa kati.
Ameviomba
vyombo vya habari kuishikilia kidete progaramu kupitia makala za magazeti,
radio pamoja na vipindi vya televisheni kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana
na masuala ya kilimo.
Comments