Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kesi inayowakabili Viongozi wa Chama cha
Demokarsia na Maendeleo (Chadema) akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe hadi
June 27 mwaka huu kwa sababu Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji
kutofika mahakamani hapo.
Hatua
hiyo imefikiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada wakili wa serikali, Faraja Nchimbi kueleza
kuwa kesi hiyo imeitishwa ili washtakiwa wasomewe maelezo ya awali lakini
mshtakiwa wa sita, Dkt.
Mashinji hayupo mahakamani.
Kwa upande wa Wakili wa utetezi, Peter Kibatala amedai kuwa Dk. Mashinji ana
udhuru yupo katika mahakama ya Songea ana kesi nyingine, hivyo wanaomba
ahirisho.
Maombi
hayo ya ahirisho yaliibua mvutano wa kisheria baada ya wakili wa serikali Paul
Kadushi kutaka kesi iahirishwe hadi kesho, huku wakili Kibatala akitaka
iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Kutokana
na mvutano huo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi June 27, mwaka huu.
Mbali ya Mbowe na Mashinji, washtakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa
Mjini Peter
Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu Bara na
Mbunge wa kibamba, John Mnyika.
Pia
mbunge wa Tarime Vijijini, John
Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa bunda, Esther Bulaya na mbunge
wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo kula njama, ambapo inadaiwa February 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la
kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.
Wanadaiwa kuwa February 16, 2018 katika barabara ya Kawawa
Kinondoni Mkwajuni washtakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani
walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Afisa wa polisi SSP, Gerald Ngiichi
kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani.
Inadaiwa
kugoma huko kulipeĺekea hofu na hatimaye kusababisha kifo cha Akwilina Akwiline
na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL
Rahim Msangi.
Comments