Changamoto za usafiri nchini Tanzania hususani katika majiji
makubwa zipombioni kupunguzwa ama kumalizika.
Hayo yamebainishwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda
kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hasssani katika mkutano
na wadau wa usafiri kutoka nchini zaidi ya 36 duniani ambao
wako hapa nchini kujadili namna sahihi ya kumaliza changamoto
za usafiri nchini Tanzania utakao fanyika kwa siku tatu kuanzia
leo jijini humo.
Alisema hawa ni wataalam walioboba katika masuala ya usafiri
ambao wameichagua Tanzania kuwa mwenyeji wao baada ya Tanzania
kupata tuzo ya kwanza katika utoaji wa huduma bora ya usafiri
barani Afrika baada ya kuanzisha usafiri wa mabasi yaendayo
kasi (UDART)ambayo kwa kiasi kikubwa yamepunguza msongamano
wa magari katikati ya jiji la Dar es Salaam na kero ambazo
miaka mitano iliyopita zilikuwa tishio.
"Moja ya changamoto za usafiri sio tu kumiliki gari au chombo
cha usafiri tatizo lipo pale ambapo ni jinsi gani ambapo
unatoka sehemu moja kwenda nyingine kwa wakati ulio kusudiwa,"
alisema Makonda.
Alisema ukiangalia hapa Dar es Salaam ongezeko la watu limefikia
Milioni 6 kwa sasa na inakadiriwa kuwa baada ya miaka 10 ijayo
watu watafikia milioni 10,hivyo ujio wa wataalamu hao wenye
uzoefu wa utatuzi wa changamoto duniani utakuwa suluhu ya matatizo
ya usafiri hususani katika jiji la Dar es Salaam na majiji mengine.
Aidha amesema awamu ya pili ya mradi ya mabasi ya mwendo kasi
kuanzia katikati ya jiji hadi mbagala itaanza mwezi wa 12 mwaka
huu na awamu ya tatu itatoka mjini kwenda uwanja wa ndege na ya
nne ni kutoka mjini hadi Tegeta na zita hitimishwa awamu nyingine
mbili hadi zifikie sita kulingana na maeneo ya jiji na baada ya
kukamilika zote hakuta kuwa tena na matatizo ya usafiri.
Kwa upande wake mwanzilishi wa mamlaka ya leseni na mjumbe
wa rufani za kodi Devid Mwaibula alisema ujio wa ugeni huo
ni fursa zaidi kwa watanzania kufanya vizuri zaidi katika
huduma ya usafiri duniani baada ya kuondokana na mifumo
ya kizamani ya kupanga rangi magari na kuweka ufito kuelekeza
ruti ambayo gari inatoa huduma na kuingia mfumo wa kisasa
zaidi wa kielektroniki .
"changamoto inayotusumbua ni ugumu wa mioyo ya madereva wasio
heshimu barabara za mwendo kasi na kuzitumia kwa matumizi yasiyo
kusudiwa,"alisema Mwaibula.
Kwa upande wake mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo kasi(BRT)
Donald Rwakatare alisema mradi wa awamu ya kwanza umeongezwa
mabasi kutoka 140 hadi 305.
Kadhalika wapo katika mchakato wa kumpata mzabuni mpya
wakuongeza mabasi mengine zaidi.
"Awamu ya kwanza imekamilika na tayari zabuni imeisha tangazwa
kwa ajili ya awamu ya pili itakayo jumuisha ruti za Mbagala hadi
kati kati ya jiji la Dar es Salaam ambayo ni kwa hisani ya
Banki ya Africa na awamu ya tatu tayari wamepata pesa ambayo
ni dola Milioni 41 kutoka Benki ya Dunia pamoja na awamu ya
nne awamu ya tano na yasita benki ya dunia itatoa pesa kwaajili
ya usanifu hivyo wanakaribisha wafadhili wengine kumalizia
mbili zilizo baki,"alisema Rwakatare.
Comments