Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania limesema mipango ya kuurejesha nchini mwili wa Askari aliyepoteza maisha baada ya kushambuliwa kwa kushtukizwa na kundi la waasi lijulikanalo kama Siriri Huko Jamhuri ya Afrika ya kati inafanywa na Umoja wa Mataifa.
Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa
Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania Kanali Ramadhani Dogoli
Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi hilo Kanali Ramadhani Dogoli ameeleza hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema licha ya kufariki askari mmoja,wengine 18 walipata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao huku kati yao askari 5 wakiwa hali zao sio nzuri.
Kanali Dogoli amesema tukio hilo limetokea Juni 3 mwaka huu ambapo kikundi cha wanajeshi Maafisa na Askari idadi yao wakiwa 90 kikiwa ni sehemu ya kikosi cha kulinda Amani kilichopo Jamhuri ya Afrika ya Kati ndipo kikakumbana na mashambulizi hayo ya kushtukizwa.
Amesema Tanzania ina vikosi vya ulinzi wa amani katika maeneo ya Lebanon,Kongo na Darfuri na kikosi ambacho kimeshambuliwa kwa kushtukizwa huko Jamhuri ya Afrika ya kati kilienda mwaka jana.
Hata hivyo amesema Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Kanda ya Umoja wa Mataifa iliyopo Bangui Mji Mkuu wa Nchi hiyo.
Comments