Baada ya kutamba na mitindo ya
nywele na nguo aina ya Kidoti brand, msichana mwenye vipaji vingi hapa nchini,
Jokate Mwegelo aimeanzisha klabu yake ijulikanayo kwa jina la Kidoti Club.
Akizungumza katika uzinduzi wa klabu
hiyo jana, Jokate alisema kuwa Kidoti Club ni tofauti na vilabu vingine
kwani katika ujio wake huo mpya, atakuwa anajihusisha na mambo mbali mbali
katika jamii husani masuala ya urembo na mitindo. Jokate pia alizindua aina
mpya ya nywele zake za kisasa katika mtindo wa kidoti Brand.
Jokate alisema kuwa kupitia klabu
yake atakuwa anatoa ushauri mbali mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa
za muziki, filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwa ajili ya rika tofauti.
Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na anaamini
watu wengi watajiunga naye.
Kwa
mujibu wa Jokate ambaye ni Miss
Tanzania namba mbili mwaka 2006, ili uwe mwanachama wa klabu hiyo,
unatakiwa
kutuma neno kidoti kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa
mbalimbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la
Kidoti
Ng’aring’ari.
“Huu ni mfumo wa kisasa katika
kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii,Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna
mtu anayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu yake, mimi pia
naelekea huko kwani nitaweka taarifa zangu mbali mbali na ili kupata lazima uwe
mwanachama,” alisema Jokate ambaye pia ni mtangazaji na mbunifu wa mavazi.
Alisema kuwa pia ataendesha
mashindano mbalimbali kwa wanachama wake na kutoa zawadi kwa washindi.
“Kama unavyojua, lengo langu
kubwa ni kutumia ujuzi na kipaji chake kwa watanzania wote, nataka wafaidike na
vipaji vyangu name kusimama mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu
yoyote, natoa wito kwa vijana wenzangu kuwa wabunifu katika kukabiliana na
masuala mbali mbali ya maisha,” alisema.
Comments