Ndugu zangu,
Nimemaliza kusoma hotuba ya Zitto
Kabwe, Kigoma, jana. Na hata baada ya kumaliza, nimebaki na kitu
ninachokiona; kuwa sasa kuna Chadema mbili mpaka pale wenye kuvutana
ndani ya Chadema watakapotuhakikishia kwa vitendo kuwa kuna Chadema
moja. Maana kwa kuyasoma haya ya Zito; "Mabadiliko ni kiu kikubwa cha
Tanzania kwa sababu mabadiliko huleta matumaini. Na kiu hii ni kubwa
zaidi kwetu sisi vijana wa kizazi hiki kipya. Siasa za kizazi kipya cha
viongozi ni siasa za majawabu ya kero za wananchi. Siasa za mabadiliko
ni siasa za kujenga na kuimarisha; ni siasa za kuaminiana na
kuheshimiana hata pale mnapopingana kimawazo. Ninataka tujenge siasa
mpya Tanzania;siasa za mabadiliko; siasa zinazojenga matumaini ya
kweli;siasa zinazowajali na kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania." -
Zitto Kabwe.
Naam, Kwa kuyasoma hayo, sasa naziona '
Chadema Mabadiliko', au labda 'Chadema - Mageuzi' na ' Chadema-
Asilia'. Naendelea kutafakari.
Ameandika hivyo Maggid Mjengwa kwenye blog yake http://www.mjengwablog.com/
Comments