Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limeandaa mechi mbili za majaribio ya matumizi ya tiketi za
elektroniki zitakazochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi ya kwanza itakuwa Desemba 26
mwaka huu saa 10 jioni ambapo itazikutanisha timu za Azam na Ruvu
Shooting. Mechi nyingine itachezwa Januari Mosi mwakani kwa
kuzikutanisha Ashanti United na JKT Ruvu.
TFF tunatoa mwito kwa washabiki
kujitokeza katika mechi hizo ambapo mbali ya kushuhudia burudani pia
watajionea jinsi mfumo huo wa tiketi za elektroniki unavyofanya kazi.
Kwa kushirikiana na benki ya CRDB
ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo ya tiketi za elektroniki, TFF
imepanga vilevile kuandaa mechi nyingine majaribio mikoani kabla ya
mfumo huanza kutumika rasmi Januari 25 mwakani katika mzunguko wa pili
wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Comments