TAARIFA KWA UMMA
KUKOMA/KUSIMAMISHWA KUWA KIONGOZI KWA MWENYEKITI WA WILAYA YA BUMBULI ndugu ABDI SHEKIMWAGA
CHADEMA Kanda ya Kaskazini, inawatangazia umma wote kuwa, Ndugu ABDI
SHEKIMWAGA amesimamishwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Bumbuli
kuanzia 21 Desemba 2013.
Ofisi ya kanda, ilipokea nakala ya taarifa na miniti ya kikao
kilichoketi tarehe 22 septemba 2013 kutoka kamati tendaji ya
wilaya/jimbo pamoja na nakala ya barua ya tuhuma alizoandikiwa ndugu
ABDI SHEKIMWAGA ili ajieleze na kujibu, ikiwemo na barua ya tarehe 12
Desemba 2013 aliyoandikiwa katibu wa mkoa kujulishwa mapendekezo na
hatua za kunusuru chama dhidi ya hila mbaya zilizokuwa zinafanywa na
ABDI SHEKIMWAGA. Kwa bahati mbaya sana ndugu SHEKIMWAGA alitoa maneno ya
kashfa na dharau pamoja na kutumia lugha isiyofaa kwa viongozi na
kuamua kugoma kujibu barua ya tuhama hizo.
Uongozi wa Kanda baada ya kupitia taarifa hizi na baada ya kufanya kikao
cha pamoja na viongozi wa wilaya tarehe 21 Desemba 2013 huko wilaya
lushoto mkoani Tanga, unamtangaza ndugu SHEKIMWAGA kuwa kwa kukinisuru
chama dhidi ya tuhuma dhidi yake, kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa
tuhuma dhidi yake, kwa ajili ya hofu na kutokuwa na imani kulikoonyeshwa
na viongozi na wanachama wenzake AMESIMAMISHWA KUWA MWENYEKITI WA CHAMA
KUANZIA TAREHE 21 DESEMBA 2013. Hatua hii ni ya kuzingatia pendekezo la
kamati tendaji ya wilaya/jimbo kwa mujibu wa ibara ya 6.3.4 (c),
“amekoma kuwa kiongozi kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa
masharti ya katiba, kanuni na maadili ua chama”.
Comments