Ufaransa
imesema mtu mwenye itikadi kali aliewahi kutiwa hatiani huko nyuma, na
ambaye alimuua afisa wa polisi na mke wake katika shambulizi la kisu
alikuwa akitekeleza wito wa kiongozi wa Dola la Kiislamu, IS.
Maafisa
nchini Ufaransa wanasema kwamba mtu mwenye itikadi kali aliewahi kutiwa
hatiani huko nyuma, na ambaye alimuua afisa wa polisi na mke wake katika
shambulizi la kisu lililohamasisha na kundi la Dola la Kiislamu,
alikuwa amebeba orodha ya walengwa mashuhuri wa mashambulizi, na
kuwahimiza wafuasi kuyageuza mashindano ya Euro 2016 kuwa "makaburi."
Shambulio
la siku ya Jumatatu katika mji mdogo kaskazini magharibi mwa Paris ni
la kwanza tangu kutokea kwa mashambulizi yaliyotekelezwa na IS mwezi
Novemba na kuua watu 130.
Kufuatia
mashambulizi hayo ya kitongoji cha Magnanville, polisi wanasema maafisa
wake sasa watapaswa kubeba silaha wakati wakiwa nje ya majukumu ya kazi
kwa ajili ya tahadhari inayoweza kujitokeza.
Katika
shambulio la usiku wa Jumatatu, mshambuliaji Larossi Abballa aliyekuwa
akifuatiliwa baada ya kutumikia kwa muda na wanajihadi, aliwaua kwa
kuwachoma kwa kisu kamanda wa polisi Jean-Baptiste na mke wake nje ya
nyumba yao.
Walengwa wa shambulio
Mwendesha
mashitaka wa Paris Francois Molins amesema kwamba Abballa anayetoka
kitongoji cha jirani cha Monte-la-Jolie aliwaambia polisi kuwa "muuaji
alisema kwamba yeye ni Muislamu na alikuwa akitimiza Ramadhan, alisema
kuwa alikuwa amekula kiapo cha utii kwa kamanda wa IS Abu Bakr
al-Baghdad wiki tatu zilizopita. Aliongeza kwa kusema alitekeleza wito
wa kiongozi huyo na namnukuu,waue makafiri nyumbani kwao na familia
zao." amesema Molins.
Dola la
Kiislamu IS limedai kuhusika na shambulio hilo la Jumatatu katika
taarifa iliyorushwa na shirika la habari la Amaq ambalo hutoa matangazo
ya kundi hilo mara kwa mara.
Polisi
wanasema kwamba waliokota orodha katika eneo la tukio yenye majina ya
polisi na wageni mashuhuri wakiwemo waandishi na wasanii kama walengwa
wa mashambulizi. Pia waligundua visu vitatu kimoja kikiwa katika lindi
la damu.
Tayari
washirika watatu wa Abballa wamekamatwa wakihusishwa na shambulio hilo,
mmoja wao aliwahi kutiwa hatiani mwaka 2013 kwa kujihusisha na mtandao
wa kusajili wapiganaji wa jihadi nchini Pakistan.
Ulinzi waimarishwa
Wakati
huo huo, polisi nchini Ufaransa wanazidi kuimarisha kikosi chao cha
usalama kwa kupeleka askari zaidi kaskazini mwa nchi hiyo pamoja na
kupanua marufuku ya pombe katika jitihada za kudhibiti vurugu zaidi
kutokea katika mashindano ya soka barani Ulaya yanayoendelea nchini
humo.
Mamlaka
bado zina wasiwasi na mashabiki wa Urusi na wale wa Uingereza, waakti
ambapo Uingereza itacheza dhidi ya Wales siku ya alhamis wakati Urusi
ikimenyana na Slovakia.
Mjini
Lille maduka yamelazimika kuacha kuuza pombe kwa saa zipatazo 60 kuanzia
Jumanne hadi Ijumaa huku baa na migahawa ikitakiwa kufungwa usiku.
Zaidi ya
wafanyakazi 2500 wa usalama wakiwemo askari polisi na wanajeshi
wamemwagwa katika mji huo kama sehemu ya tahadhari ikiwa patatokea
vurugu zingine.DW
Comments