OBAMA KUTOHUDHURIA MAZISHI YA MUHAMMAD ALI KESHOKUTWA
Rais wa Marekani Barrack Obama hatohudhuria mazishi ya marehemu Muhammad Ali siku ya Ijumaa,kulingana na Ikulu ya rais.
Ali alifariki Ijumaa iliopita akiwa na umri wa miaka 74 katika hospitali moja huko Phoenix, Arizona.
Viongozi duniani watakuwa miongoni mwa maelfu watakaohudhuria mazishi hayo yatakayofanyika katika eneo la Louisville,Kentucky ambapo Ali alizaliwa.
Ikulu ya White House imesema bw Obama na mkewe Ali, Lonnie walizungumza kwa njia ya simu.
Miongoni mwa wale watakaohudhuria ni rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mfalme Abdullah wa Jordan.
Aliyekuwa bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Lennox Lewis na muigizaji Will Smith ambaye aliigiza kama Ali ni miongoni mwa wale watakaobeba jeneza lake.
Comments