Michuano ya Euro 2016 inaanza rasmi leo nchini Ufaransa ambapo
kutakuwa na mchezo mmoja unaohusisha wenyeji Ufaransa watakapambana
vikali na Romania katika mchezo utakaopigwa kunako dimba la Stade de
France majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Kama ilivyoada katika michuano ya Ulaya, Amerika na hata dunia kwa
ujumla huwa kunakuwa na mpira maalum uliondaliwa kwa ajili ya michunao
husika.
Katika michuano ya Euro mwaka huu, mpira utakaotumika unajulikana kwa
jina la Adidas Beau Jeu. Beau Jeu ni jina la kifaransa lenye maana ya
‘Beautiful Game’ au ‘Beautiful Play’ ambapo kwa Kiswahili maana yake ni
Mchezo mzuri.
Huu ulizinduliwa na Adidas na kutambulishwa na mchezaji wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane mwezi Novemba mwaka jana.
Mpira huu unajumuisha baadhi ya vitu kama Adidas Brazuca. Una rangi
ya bluu, nyeusi na machungwa huku ukiwa umeandikwa ‘EURO 2016’.
Comments