Kiungo wa zamani wa AC Milan, Gennaro Gattuso ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo baada ya Vincenzo Montella kutimuliwa kufuatia mwenendo mbaya msimu huu katika Ligi Kuu ya Italia - Seria A.
Licha ya usajili wa bei mbaya uliofanywa na wamiliki wapya matajiri wa Kichina, AC Milan iko nafasi ya saba kwenye msimamo wa Seria A, ikiwa imeachwa kwa pointi 18 na vinara Napoli.
Comments