Na Mwandishi Wetu
TAKWIMU zinaonesha kwamba, kati ya wanawake 10,0000, wanawake 32,000 hufariki kutokana na ugonjwa wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi.
Waziri wa Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikabidhiwa vifaa tiba na vya kufundishia watoa huduma vya ugonjwa wa saratani ya Mlango wa shingo ya Kizazi jijini Dar es Salaam.
Pia amewaelekeza waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuanzisha zoezi la wazi la uchunguzi wa saratani ya kizazi angalau mara moja katika mwezi ili kusaidia kutokomeza tatizo hilo nchini.
Akizungumza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alipokuwa akipokea vifaa tiba na vifaa vya kufundishia watoa huduma za afya vya ugonjwa wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi na matiti vyenye thamani ya sh.milioni 98 vilivyotolewa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na Jhpiego.
“Takwimu zinaonesha kati ya wanawake 10,0000, vifo 32,000 vinavyotokana na saratani ya mlango wa kizazi hutokea na wanaopona ni wacache,” amesema Waziri Ummy.
Aidha amesema kutokana na hali hiyo Serikali imejipanga kuhakikisha hadi kufikia Desemba, 2018 kufikia wanawake milioni 3 kuwapima na kujua kama wanaviashiria vya awali vya ugonjwa huo ili waanze matibabu.
Ameongeza kuwa serikali imejipanga pia kuhakikisha ifikapo Desemba, 2018, kila kituo cha afya cha serikali kiwe kinatoa huduma za matibabu ya Saratani ambapo hadi sasa kati ya vituo 524 ni vituo 255 pekee vinavyotoa huduma hiyo.
Waziri Ummy ameendelea kusisitiza kwa kuwataka Wanganga wakuu wa Mikoa kuhakikisha vituo vyao vya afya vinatoa huduma hiyo bure.
Aidha amewahimiza wanawake kujitokeza katika vituo vya afya kufanyiwa vipimo ili wakibainika kuwa na viashiria vya ugonjwa huo waanze matibabu.
Kwa upende wake Mkurugenzi wa Jhpiego Jeremie Zoungrana amesema msaada huo waliotoa ni kwa ajili ya kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano katika kupambana na vifo vya wanawake vinavyotokana na saratani.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments