Mkurugenzi wa Aga Khan Foundation na Taasisi ya maendeleo ya Binadamu, Profesa Kofi Marfo(wakatikati),Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU), Profesa Joe Lugalla(wakwanza kushoto) wakizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam
Na Mariamu Muhando Dar es salaam
Imeelezwa kuwa zaidi ya watoto milioni 250 ulimwenguni wameshindwa kupata matibabu ya utapiamlo kutokana na umasikini katika kipindi cha miaka ya mwanzo tangu mtoto kuzaliwa .
Hayo yamebainishwa katika maadhimisho Mkutano wa Kimataifa wa kujadili malezi na makuzi ya watoto uliomalizika leo jijini Dar es Salaam ambapo wasomi,na watafiti kutoka nchi mbalimbali wameshiriki kwenye mkuano huo.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Aga Khan Foundation na Taasisi ya maendeleo ya Binadamu, Profesa Kofi Marfo, amesema kuwa ni wajibu wa maendeleo ya watoto hutegemea kila mtu kuanzia wazazi, jamii hadi Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU), Profesa Joe Lugalla amesema vyuo vyote vinapaswa kuonyesha uhusiano bora kwa jamii ili viweze kuleta huduma za mipango ambazo zitaimarisha misingi ya maendeleo ya binadamu.
Mkutano huo umefanyika kwa muda wa siku tatu umeandaliwa na Taasisi ya Chuo Kikuu cha Aga Khan, Taasisi ya Maendeleo ya Binadamu (IHD) kwa kushirikiana na The Conrad Hilton Foundation.
Comments