STAA wa soka nchini England, Wayne Rooney amefanikiwa kurejesha ndoa yake na Coleen ambayo ilikuwa inaelekea kuvunjika kufuatia matendo yake ya ovyo nje ya uwanja.
Colleen ameliambia gazeti la Daily mail la nchini Uingereza kuwa wameamua kuanza upya na kusahau yote yaliyotokea kipindi cha nyuma bila kujali magazeti yalizungumza kiasi gani juu yao.
Wayne alihukumiwa kutoendesha gari na kutofanya kazi za kijamii baada ya kukamatwa akiwa anaendesha gari amelewa huku akiwa na mwanamke kwenye usafiri huo.
Imekuwa ni kawaida kwa Rooney kupiga ulabu na kwenda kubeba makahaba kwenye madanguro nyakati za usiku.
Coleen mwenye miaka 31, alichukizwa na kitendo hicho na alikuwa mbioni kutaka kuivunja ndoa yake na Rooney.
Comments