Skip to main content

SERIKALI YA OMAN YAVUTIWA NA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI TANZANI



 Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda akizungumza jambo na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. AL Mahruqi walipokutana leo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi akizungumza jambo na Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda alipomtembelea Ofisi kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Bibi. Zainabu Chaula(kushoto) wakimuonyesha Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi kifungu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 kinachozungumzia utoaji  wa huduma za jamii alipotembelea Ofisi za Naibu Waziri wa huyo leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi (wa pili kutoka kulia) alipotembelea Ofisi za TAMISEMI Jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Bi. Debora Mkemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Bibi. Zainabu Chaula pamoja na mmoja wa Afisa kutoka Mambo ya Nje ya Nchi Bw. Odiro. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO)


Na Eliphace Marwa
BALOZI wa Oman Ali Al Mahruqi amesema Wafanyabiashara wa nchi hiyo wamevutiwa na na hatua mbalimbali znazochuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kujenga mazingira bora kwa wawekezaji na wengi wao wapo mbioni kuja kuwekeza katika miradi mikubwa ya maendeleo nchini.

Balozi Al Mahruqi aliyasema hayo leo aJijini Dar es Salaam wa mazungumzo baina yake na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Kakunda na kuongeza kuwa suala la usalama wa mitaji yao ni jambo ambalo Wafanyabiashara hao wanapenda kuhakikishiwa na Serikali ya Tanzania.
Balozi Mahruqi alisema miongoni mwa fursa zinazowavutia Wafanyabiashara wa Oman kuja kuwekeza nchini ni pamoja na ubora wa miundombinu katika sekta za elimu na mifugo ikiwemo upatikanaji wa tasnia ya nyama.
“Serikali ya Oman ina mpango wa kuja kuwekeza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kipaumbele kikubwa kitakuwa ni nchi ya Tanzania kutokana na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Tanzania,” alisema   Balozi Mahruqi.
Aidha Balozi Mahruqi aliitaka Serikali kuharakisha makubaliano ya mikataba baina ya Mataifa hay ili kuwezesha wawekezaji kutoka Oman kupata fursa ya kuwekeza nchini na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kutoka Oman.
Kwa upande wake Naye Naibu  Waziri Kakunda alimuahidi Balozi Mahruqi kufanyia kazi changamoto zilizopo ili kuhakikisha wawekezaji kutoka Oman wanakuja kwa wingi kuwekeza nchini bila ya kuwa na hofu ya usalama wa mitaji yao.
“Nitafuatilia kwa kina kwa wataalamu weu wanaohusika na uwekezaji kwenye kiwanda cha nyama ambapo wawekezaji kutoka Oman watawekeza takribani dola milioni tatu ambazo zitasaidia wafugaji wa Watanzania kupata soko la mifugo yao” alisema Naibu Waziri Kakunda.
Aidha Kakunda aliahidi kufuatilia maeneo ambayo Serikali ya Oman iliahidi kusaidia kaika ujenzi wa visima mia moja vya maji katika maeneo ya mashule ili kupata orodha kamili ya shule zinazotakiwa kupatiwa msaada huo.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...