Wakandarasi katika halmashauri Ilala wametakiwa kutumia vifaa vya kisasa katika kusafisha maeneo yao
Naibu Meya wa manispaa ya Ilala Omari Kumbilamoto(picha na mtandao)
Katika kuifanya halmashauri ya Ilala jijini Dar es Salaam kuwa safi na ya kuvutia wakandarasi katika halmashauri hiyo wametakiwa kutumia vifaa vya kisasa katika kusafisha maeneo wanayoyasimamia.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Diwani wa kata ya Vingunguti na naibu Meya wa manispaa ya Ilala Omari Kumbilamoto wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kurejea kwake hapa nchini akitokea nchini Dubai ambapo alikuwa nchini humo kwa takriban wiki mbili kwa lengo la kujifunza namna ambavyo manispaa za miji mingine zinavyoweza kutekeleza majukumu yake .
Aidha Kumbilamboto akizungumzia kuhusu kata ya vingunguti amesema kata hiyo imeweza kutatua changamoto wanazokabiliana nazo kwa asilimia tisini huku akilipongeza jeshi la polisi kwa kutoa mafunzo kwa walinzi shirikishi katika kata hiyo ambayo yamefanikisha usalama kwa watu wapitao usiku wakielekea machinjioni.
Diwani huyo wa kata ya vingunguti na naibu meya wa manispaa ya Ilala amewataka wakazi wa kata hiyo kuongeza umoja na mshikamano baina yao na kutokuingiza itikadi za vyama vyao katika masuala ya maendeleo.
Comments