Unapokuwa faragha na mpenzi wako, kuna baadhi ya mambo unatakiwa kuyaepuka kwani yanaweza kutibua hali ya hewa na mwishowe kutopata ile furaha mliyodhamiria. Achilia mbali hayo ya kufanya, pia kuna maneno ambayo unatakiwa kujichunga sana kutoyatamka pale unapokuwa kwenye uwanja wa kujidai na mpenzi wako.
Haya nayo madhara yake ni makubwa kwani yanaweza hata kuufanya uhusiano wenu ukafikia tamati. Maneno hayo 8 ni haya yafuatayo;
1.Sitaki hivi na vile
Unapokuwa faragha na mpenzi wako hutakiwi kugomea vitu ambavyo mpenzi wako anataka kukufanyia tena kwa ukali. Kwa mfano, kuna baadhi ya wanawake wanaposhikwa maeneo flani ya miili yao husema; ‘bwana mi staki, mwenzio unanichanganya’.
Sentensi hiyo inapotolewa kimahaba haina madhara na inaweza kunogesha mambo kwani inaeleweka mwanamke anaposema hivyo anamaanisha nataka sitaki, lakini unapomwambia mpenzi wako sitaki hiki tena kwa lugha ya ukali ukimaanisha unachokisema, unaweza kuharibu mambo.
2. Hivyo siyo vizuri
Unamwambia mpenzi wako kwa macho makavu kuwa anavyokufanyia siyo vizuri? Hapana, hiyo siyo poa. Hata kama uko ‘streiti’ lakini tafuta njia nyingine ya kumfikishia ujumbe huo bila kumharibia ‘mudi’ yake kwani wanaume si watu wanaopenda kukosolewa katika kila jambo.
3.Siyo mkali uwanjani
Unaweza kujikuta umeangukia kwa mwanaume ambaye hayajui ‘majamboz’, yaani wewe ndiye unayechukua muda mwingi kumuelekeza afanyeje ili muipate furaha.
Hilo siyo suala la kukufanya uanze kumlaumu na kufikia hatua ya kumchana laivu kuwa yeye siyo mkali. Mvumilie, endelea kuwa naye huku ukiamini siku moja atakuwa mzoefu. Fahamu kuwa, kisaikolojia ukimwambia siyo mzuri faragha ndiyo unazidisha tatizo na anaweza kuona ni bora asiwe na wewe kabisa ili kukwepa kuumbuka.
4. Wewe siyo mtundu kama x-dear wangu
Kwanza unatakiwa kujua kuwa, uwapo faragha hutakiwi kuuzungumzia uhusiano wako uliopita, kwa kuufananisha au kuutofautisha. Hivyo hutakiwi pia kumwambia mpenzi wako kuwa yeye siyo mtundu kama mpenzi wako wa zamani. Ukimwambia hivyo utamfanya ahisi ipo siku unaweza kumuacha na kumrudia wa zamani, mazingira ambayo siyo mazuri.
5. Ingekuwa yule wangu wa zamani angenifanyia hivi
Kwa mfano mpenzi wako hataki kukufanyia kitu flani ambacho uliwahi kufanyiwa na mpenzi wako wa zamani, hutakiwi kuwa muwazi katika hilo. Cha kufanya akishaonesha hataki kukufanyia hicho kitu, mpotezee kisha endeleeni na mambo mengine, wala usimkumbushie kuwa ingekuwa mpenzi wako wa zamani angekufanyia.
6. Mbona hufanyi sahihi
Kweli anaweza kufanya mambo katika njia ambayo unaona siyo sahihi kwako lakini huna sababu ya kuwa mkali, mwelekeze namna unavyotaka afanye tena kwa upole kwa kutumia lugha ya kimahaba.
7. Hii inaboa, unaniboa
Hata kama ndiyo ukweli wenyewe lakini unapokuwa faragha na mpenzi wako epuka kumwambia anakuboa au anafanya mambo yanayokuboa. Ukimtamkia hivyo, wewe utakuwa umemboa zaidi na furaha lazima itoweke.
8. Jina la mwanaume mwingine
Dah!Kama unataka siku hiyo hiyo uachwe, jaribu kutaja jina la mwanaume mwingine wakati uko faragha na mpenzi wako. Ni mbaya sana kwani unaonesha unamuwaza sana yeye kuliko mpenzi wako.
Katika hili nalo unatakiwa kuwa makini. Hayo ndiyo baadhi ya maneno ambayo unatakiwa kutumia gharama yoyote kuyaepuka unapokuwa faragha na mpenzi wako.
Tambua penzi linashikiliwa na vitu vidogovidogo sana ambayo unaweza kuvidharau lakini madhara yake yakawa makubwa. Kwa maana hiyo, hakikisha kila neno unalotaka kulitoa mdomoni mwako kwenda kwa mpenzi wako unalipima kwanza, usipofanya hivyo unaweza kuja kujuta siku moja. chanzo:bongo hot zone
Comments