Dk Slaa enzi akiwa Katibu Mkuu wa Chadema (Picha na Maktaba) |
Aliyekuwa Katibu Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt.
Wilbroad Slaa amezungumzia hatua aliyoichukua Rais John Magufuli kumteua kuwa
Balozi.
Dkt. Slaa amesema ubalozi ni nafasi ambazo zipo katika himaya ya Mkuu wa Nchi
hivyo bila shaka hadi Rais kufikia hatua ya kumteua atakuwa na sababu za uteuzi huo.
“Hatimaye kama ni mapenzi wa Mungu namshukuru kwa uteuzi huo ninachoweza
kusema katika hatua hii ni kwamba ni wajibu mkubwa katika kipindi hiki cha
kujenga taifa letu. Kama ni kutoa mchango wangu nitakuwa tayari kutoa,
Mwenyenzi Mungu akinisaidia” Dkt. Slaa amekiambia kituo cha runinga
cha Azam.
Hapo jana November 23, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Rais Dkt. John Magufuli alimteua Dkt. Wilbroad Slaa kuwa Balozi na inatarajiwa
ataapishwa pindi taratibu zikikamilika.
Comments