Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Kinondoni Ibrahm
mwaipopo amesema kuwa wanauhakika wa kupata ushindi kata ya Mbweni iliyopo
katika wilaya hiyo.
Hali hiyo imekuja kufuatia Tume ya Taifa ya uchaguzi kutangaza kufanyika
kwa Uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 za Tanzania Bara.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, leo amezindua kwa kishindo kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Mbweni, Wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, akifuatana na viongozi mbalimbali wa Chama akiwemo Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe.
Pichani, Mpogolo akimnadi mgombea wa Udiwani katika Kata hiyo kwa tiketi ya CCM, Hashim Mbonde katika mkutano uliofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya afisa Mtendaji Kata ya Mbweni. Kumradhi, Kutokana na muda hatukuweza kuweka maelezo kwenye picha zote, tafadhali pitia moja baada ya nyingine utapata taswira nzima ya shughuli hiyo nzito. Picha zote na Bashir Nkoromo
Akizungumza na mwandihi wa habari hizi Dar es Salaam jana Mwaipopo alisema
kuwa kwa sasa kampeni za uchaguzi zilisha anza na wamekuwa wakifanya
kampeni hizo katika hali ya utulivu na moja ya vipaumbele kwa wakazi
wa Mbweni katika kampeni ni tumeahdi kuwapatia maji wananchi.
"Tulianza kampeni mara tu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutangaza uchaguzi
mdogo wa Madiwani kufanyika kata 43 za Tanzania Bara na tayari tumeanza
kutatua kero ya maji kwa wakazi wa kaka ya Mbweni,"alisema Mwaipopo.
Alisema kuwa baada ya uchaguzi mkuu wa 215 kuwa umemalizika tayari
katika wilaya yake ya Kinondo walisha weza kufanya chakuzi zingine
za mitaa na CCM iliibuka mshindi kwa kuwagalagaza wapinzani wao
katika mtaa ambapo katika uchaguzi ujao Mbweni wanauhakika wa kushinda
kwa kuwa sera nzuri na utekelezaji wa malengo wamekuwa wakifanya
katika kuhudumia wananchi kama chama kinacho ongoza serikali ya awamu ya
tano.
Kwa kuzingatia mashart ya vifungu vya sheria, sheria ya kifungu cha 13(3) cha
uchaguzi ,sheria ya serikali za mitaa ,sura ya 292 imetaja uchaguzi wa
kujaza nafasi wazi za madiwani zinapotokea kwa njia ya uchaguzi angalau
mara mbili katika kipindi cha mwaka wa kalenda.
Comments