Naibu mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Julias
Na Mussa.N.Khalid
Taasisi ya kuzuia na
Kupambana na Rushwa NCHINI TAKUKURU imewataka watanzania kuonyesha ushirikiano
wa kumtafuta mmoja kati ya wafanyakazi wa TAKUKURU Godfrey John Lugani kutokana
na kosa la kujikusanyia mali pasipo kutoa maelezo ya mali hizo.
Hayo yameelezwa leo na
Naibu mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Julias wakati
akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam ambapo amesema kwa mujibu wa
sheria ya kupambana na rushwa ni kosa la jinai kwa mtumishi kuwa na mali ambazo
zimezidi kipato chake.
Brigedia Jenerali John
amesema kutokana na hilo wanaendelea kumtafuta Godfrey popote pale alipo ili
aweze kutoa taarifa kamili ya kwa kuweza kutumia ofisi kwa matumizi mabaya kwa
kuweza kujikusanyia mali nyingi hivyo
amewataka watanzania kutoa taarifa pindi watakapo baini kuwa anakosa hilo.
Amesema mali ambazo Godfrey amejikusanyia kuwa ni
pamoja na nyumba za kifahari za gorofa magari,pamoja na viwanja katika maeneo
mbalimbali nchini.
Hata hivyo Brigedia Jenerali John ametoa angalizo kwa watumishi wote wa umma kuwa ni kosa kujipatia mali nje
ya utaratibu wa serikali na hivyo watakaobainika watawachukulia hatua kali za
kisheria ili mali za serikali ziweze kuwa salama.
Comments