Wadau wa mifugo imeshauriwa kuweka mazingira mazuri kwa sekta ya mifugo ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mifugo.
Wadau wa sekta hiyo wamesema hayo Dar es Salaam Jumanne Novemba 28,2017 wakati wa uzinduzi wa mkakati wa ushawishi wa sera ya mifugo ulioandaliwa na jukwaa lawadau wa kilimo (Ansaf)ambapo wametaka Serikali ihakikishe wafugaji wanafanya shughuli zao katikamaeneo yanayoeleweka na si kuhamahama kama ilivyo sasa.
Hadi sasa sekta ya ufugaji inatajwa kama sekta inayokuwa kwa kasi ya asilimia 5o hapa nchini hapa huku Tanzania ikitajwa kuwa ni nchi ya tatukwa kuwa na wanyama wanaofugwa baada ya nchi za Ethiopia na Sudani.
Katibu mkuu wa chama cha wafugaji nchini, Magembe Makoye amesema kuhamahama wafugaji kunasababisha ufugaji usio na tija na manufaa kwa viwanda, hivyo sekta hiyo kuendelea kuendeshwa kwa mazoea.
“Hatuwezi kuzungumzia ufugaji wa tija au uchumi wa viwanda kama wafugaji wataendelea kuzunguka na kuhamahama. Muhimu wahakikishiwe usalama na utulivu wafanye shughuli zao, itakuwa rahisi hata kuwashawishi wawekezaji kuwekeza kwenye sekta hii,” amesema.
Mjumbe wa bodi ya maziwa, Charles Tumaini amelalamikia urasimu uliopo katika uanzishaji wa viwanda hali inayowakatisha tamaa vijana wenye lengo la kuanzisha viwanda vidogovidogo.
“Tunaposema Tanzania ya viwanda lazima malighafi ziwe za ndani, utakuta mtu ana kiasi chake kidogo cha fedha anataka kuanzisha kiwanda cha kusindika maziwa atakutana na vikwazo hadi asitishe wazo hilo.”Amesema.
“Hatuwezi kupiga hatua kwa idadi hii ya viwanda tulivyonavyo. Viwanda vilivyopo vina uwezo wa kusindika lita 700,000 kwa mwezi lakini vinapata lita 200,000 pekee. Tuone hii ni changamoto tunayotakiwa kuifanyia kazi,” amesema.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Maria Mashingo naye alisema wakati umefika kwa wafugaji kuacha kufuga kwa mazoea na kuangalia zaidi biashara.
Amesema mkakati wa miaka 10 wa wizara hiyo unaonyesha kutakuwa na ongezeko la mahitaji ya nyama, hivyo ni muhimu kwa wafugaji kuchangamkia fursa hiyo.Dk Mashigo ameomba wakala wa misitu kuruhusu majani yaliyopo misituni kutumika kwa malisho ya mifugo.
wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge amesema mkakati uliozinduliwa unalenga kuhamasisha ushiriki wa wawekezaji kutoka sekta binafsi.
Wakati hayo yakitajwa leo sekta ya ufugaji inatazamiwa kujangia maendeleo ifikapo mwaka 2020 sensa hadi sasa inasemwa kuwa sekta ya ufugaji imechangia takribani asilimia 7:47 mpaka 10.
Comments