Katibu Mkuu Wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto DR Mpoki(kushoto) Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mhe. Dkt. Detlef Wachter wakionyesha vifaa kwa ajili ya kutolea huduma za matibabu kwa watoto njiti
Zaidi ya watoto njiti laki 236 elfu waliozaliwa katika kipindi kilichoanzia mwaka 2015 kati yao watoto 9,400 wamefariki kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokua na ujuzi wa namna ya kuwahudumia pamoja ukosefu wa vifaa vya kuwahudua hapa nchini.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya Maadhimisho ya Siku Ya Mtoto Njiti Duniani ambapo Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto imekabidhiwa Vifaa mbalimbali vitakavyotumika kutoa huduma ya kuwahudumia watoto hao msaada uliotolewa na taasisi ya Mradi wa kusaidia Afya Tanzania kutoka nchini Ujerumani GIZ.
Akizungumza katika Maadhimisho hayo jana Katibu Mkuu Wa Wizara hiyo DR Mpoki Ulusibisya amsema watotot wanao zaliwa bila ya kutimiza siku zao ndio wanao changia ongezeko la vifo vya watoto wachanga ambapo shirika hilo limeona Mkoa wa Mtwara na Lindi imekuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa vifaa hivyo na kusema kuwa vifaa hivyo vitasambazwa katika Mikoa hiyo.
Aidha DR MPOKI amsema GIZ imeweza kutoa mafunzo Afya ya muda wa miaka miwili kwa watumishi wa Afya kwenye vituo vya kutolea huduma huku akielezea namna ambayo vifaa hivyo vitavyo weza msadia mtoto njiti
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara DR WEDSON SICHALWE amesema hali ya vifo kwa watoto wachanga imekuwa ni mbaya ambapo asilimia 25 kila mwaka katika mkoa wa Mtwara wanazaliwa watoto wenye uzito mdogo.
Comments